Tarehe 6 Septemba, 2024, Mhe. Balozi Lt Gen Mathew Edward Mkingule alimpokea Balozi wa Algeria nchini Zambia Mhe Tewfik Abdelkader aliyeutembelea Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Zambia kwa ajili ya kujitambulisha na kuimarisha uhusiano wa Kiofisi katika eneo la Uwakilishi.

Balozi Abdelkader alifanya ziara ya kujitambulisha kwa Balozi Mkingule ikiwa ni sehemu ya Utamaduni wa Mabalozi mara baada ya kuwasilisha Hati zake za Utambulisho katika Mamlaka za Jamhuri ya Zambia. Balozi Abdelkader aliwasilisha shukrani kwa mapokezi mazuri pamoja na ukarimu anaopata kutoka kwa Waheshimiwa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini Zambia.

Balozi Mkingule alimpatia ahadi ya ushirikiano awapo nchini Zambia ikipa ni pamoja na kushirikiana katika masuala ya uwili pamoja na Umoja wa Afrika. Balozi Abdelkader ameonesha shauku ya kujifunza Lugha ya Kiswahili ambayo tayari imeanza kufundishwa nchini Zambia kupitia Chuo Kikuu cha Zambia kwa ushirikiano na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.