Tarehe 12 Septemba, 2024 Mhe Balozi Lt Gen Mathew E Mkingule alishiriki Kikao cha Mabalozi kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Southern African Development Community - SADC). Kikao hicho kiliitishwa na Ubalozi wa Jamhuri ya Zimbabwe kwa lengo la kuimarisha umoja wa Mabalozi wa Kundi la SADC wenye makazi Lusaka nchini Zambia pamoja na kuangazia masuala muhimu ya Jumuiya hiyo mara baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC uliohitimishwa nchini Zimbabwe mwezi Agosti 2024.