Tarehe 5 Septemba 2024 ujumbe kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) ulitembelea Ofisi za Ubalozi mara baada ya kuhitimisha ziara yao ya kikazi nchini Zambia. Ujumbe huo ulipokelewa na kufanya mazungumzo mafupi na Mhe Balozi Lt Gen Mathew Edward Mkingule katika Ofisi za Ubalozi zilizopo Mtaa wa Umoja wa Mataifa, Lusaka.