Baadhi ya Viongozi wa Diaspora wamefika Ubalozini kwa ajili ya kikao na Mhe. Balozi Lt Gen Mathew Edward Mkingule. Kupitia Kikao hicho, Balozi Mkingule aliwahimiza kudumisha umoja, ushirikiano na upendo ndani ya Jumuiya ya Watanzania waishio nchini Zambia. Pamoja na mambo mengine, Viongozi hao wameahidi kuijenga Jumuiya Bora itakayozingatia misingi ya uwazi, ukweli, haki na uwajibikaji ili kufikiano malengo ya uanzishwaji wa Jumuiya hiyo.