Wanadiplomasia wa nchi za Afrika chini ya Mabalozi wa Nchi zenye uwakilishi wa makazi Lusaka, Zambia wamejumuika kwa hafla fupi ya kuwaaga Wanadiplomasia wa nchi za Afrika waliomaliza muda wao pamoja na kuwakaribisha Wanadiplomasia wapya kutoka nchi za Afrika. Hafla hiyo ilitoa fursa ya kubadilishana mawasiliano pamoja na kuimarisha uratibu wa shughuli za Uwakilishi.