Maadhimisho ya Pili ya Kiswahili Duniani mwaka 2023 nchini Zambia yalihusisha tukio la utiaji saini Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano kati ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Chuo Kikuu cha Zambia katika Taaluma pamoja na Ufundishaji wa Lugha ya Kiswahili nchini Zambia. Ujumbe kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam uliongozwa na Profesa Bonaventure Rutinwa, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho anayesimamia Taaluma.

Maadhimisho hayo yalihudhuriwa na Wanazuoni na Wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Zambia; Wawakilishi kutoka Wizara na Taasisi za Umma za Jamhuri ya Zambia; Waheshimiwa Mabalozi kutoka nchi zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), na Soko la Pamoja la Mashariki na Kusini mwa Africa (COMESA); Chemba za Biashara na Viwanda; Diaspora ya Tanzania nchini Zambia; Wahariri na Waandishi wa Habari wa Vituo vya Habari vya Televisheni, Redio, Magazeti na Blogi mbalimbali