Tarehe 24 Oktoba 2023 , Jamhuri ya Zambia ilihitimisha miaka 59 ya uhuru wake ambapo Rais Samia Suluhu Hassan alipewa heshima ya kuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho hayo ambayo huenda sambamba na uwekaji wa mashada ya maua katika Mnara wa Kumbukumbu ya Mashujaa waliopigania uhuru wa Zambia  pamoja na hafla fupi ya utoaji wa tuzo na nishani mbalimbali kwa Wananchi waliotambuliwa kwa kujitoa kwa Taifa la Zambia.