Tarehe 14 Julai, 2023 Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Zambia kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Zambia ulifanya Maadhimisho ya Pili ya Kiswahili Duniani chini ya Kaulimbiu “KISWAHILI NI ZAIDI YA LUGHA”. Mgeni rasmi katika Maadhimisho hayo alikuwa Mhe. Douglas Syakalima (Mb.), Waziri wa Elimu wa Jamhuri ya Zambia. Maadhimisho hayo ya Pili ya Kiswahili Duniani yalifanyika sawia na tukio la utiaji saini Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano kati ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Chuo Kikuu cha Zambia katika Taaluma pamoja na Ufundishaji wa Lugha ya Kiswahili nchini Zambia.