Balozi wa Tanzania nchini Zambia Mhe. Lt Gen Mathew Edward Mkingule aliambatana na Mama Balozi Frida Mathew Mkingule,  baadhi ya Watumishi wa Ubalozi na Watanzania waishio nchini Zambia katika Mapokezi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. Katika mapokezi hayo, Ofisi ya Shirika la Ndege la Tanzania - Lusaka lilitoa ukaribisho maalum kwa Mheshimiwa Rais Samia kupitia Bango lililowekwa katika kipita shoto - eneo la Water Falls kwenye Barabara ya Great East, Lusaka.