Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amewasili nchini Zambia tarehe 23 Oktoba 2023 kwa Ziara ya Kitaifa ya Siku tatu na kupokelewa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Zambia Mheshimiwa Hakainde Hichilema. Miongoni mwa matukio ya kihistoria yanayotarajiwa kufanyika wakati wa ziara ya Rais Samia ni pamoja na kuwa mgeni rasimi katika Sherehe za Maadhimisho ya miaka 59 ya Uhuru wa Jamhuri ya Zambia sambamba na heshima kubwa aliyopewa ya kulihutubia Bunge la Jamhuri ya Zambia akiwa ni Rais wa Kwanza wa Afrika katika kipindi zaidi ya miaka kumi iliyopita kulihutubia Bunge hilo.