Ziara ya Kitaifa ya Rais Samia Suluhu Hassan nchini Zambia imefana kwa mapokezi makubwa yaliyoandaliwa na Serikali ya Jamhuri ya Zambia. Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Kimataifa wa Kenneth Kaunda jijini Lusaka, Mhe. Rais Samia alipata mapokezi rasmi yaliyofanywa na mwenyeji wake Rais wa Zambia Mhe. Hakainde Hichilema. Katika mapokezi hayo, Mhe. Rais Samia alikagua gwaride maalum lililoandaliwa kwa ajili yake pamoja na kupigiwa mizinga 21.