Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Malori Tanzania (CHAWAMATA), Bw. Greyson Wimile ameongoza viongozi wa Chama hicho kutembelea Ofisi za Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Zambia ambapo walipata fursa za kufanya mazungumzo na Balozi Lt Gen Mathew Edward Mkingule. Pamoja na mambo mengine,  Bw. Wimile aliufahamisha Ubalozi kuwa wapo nchini Zambia kushiriki Mkutano wa Vyama vya Madereva na Wafanyakazi kwenye Malori wa nchi za SADC.